HOSPITALINI NILIPOWAKUTA MALAIKA: SEHEMU YA KWANZA
Nilikuwa katika hali ambayo singalijua. Siwezi kamwe ambatanisha yaliyokuwa yakitendeka isipokuwa tu ninayo mawazo ya mwili wangu mzima kutetemeka. Jambo la mwisho ninalokumbuka ni mama yangu mzazi akiniuliza, "My son, mbona watetemeka kama jino la nyanya mzee"? Hapo pengine nilijipata hospitalini nilipopata nafuu baada ya wiki tatu. Nilijihisi vyema baada ya wiki tatu nilipoyafungua macho yangu na kujipata nimelazwa kitandani cha zahanati moja huko sehemu za Meru. Kando yangu walikuwa watu kadhaa wengi wao wenye nyuso zenye huzuni. Kati yao alikuwepo shangazi yangu aliyekuwa akijitahidi na maombi. Pia walikuwemo marafiki zangu, dada yangu na pia binti mrembo ambaye kwa sasa ni bibi yangu. Nipomtazama dada yangu, machozi yalianza kutiririka tiritiri kama maji ya Mto Ruiru. Lakini kwa njia, ya kumfinyia macho, nilimuhakikishia na kumuthidhibitishia ya kwamba nitapata nafuu kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu. Punde katika ile hali ya kuhuzunika, daktari wa jinsia y...