HOSPITALINI NILIPOWAKUTA MALAIKA: SEHEMU YA KWANZA
Nilikuwa katika hali ambayo singalijua. Siwezi kamwe ambatanisha yaliyokuwa yakitendeka isipokuwa tu ninayo mawazo ya mwili wangu mzima kutetemeka. Jambo la mwisho ninalokumbuka ni mama yangu mzazi akiniuliza, "My son, mbona watetemeka kama jino la nyanya mzee"? Hapo pengine nilijipata hospitalini nilipopata nafuu baada ya wiki tatu.
Nilijihisi vyema baada ya wiki tatu nilipoyafungua macho yangu na kujipata nimelazwa kitandani cha zahanati moja huko sehemu za Meru. Kando yangu walikuwa watu kadhaa wengi wao wenye nyuso zenye huzuni. Kati yao alikuwepo shangazi yangu aliyekuwa akijitahidi na maombi. Pia walikuwemo marafiki zangu, dada yangu na pia binti mrembo ambaye kwa sasa ni bibi yangu. Nipomtazama dada yangu, machozi yalianza kutiririka tiritiri kama maji ya Mto Ruiru. Lakini kwa njia, ya kumfinyia macho, nilimuhakikishia na kumuthidhibitishia ya kwamba nitapata nafuu kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu.
Punde katika ile hali ya kuhuzunika, daktari wa jinsia ya kike alifika pale kando ya kitanda changu. Bali ya mimi kugonjeka, niliweza kuutazama urembo wa huyo daktari. Umbo lake lilikuwa la kutamani na kumezea mate. Daktari msichana mwenye rangi nyeupe kama pamba. Mrembo kweli kweli mwenye miguu mrefu kama korongo. Nilijikakamua kimwanaume nikapindua shingo na kumuuliza, "Daktari, mbona nimelazwa hospitalini"? Kimya kikatanda kati ya wageni wangu wote wakingoja kwa hamu na gamu kupokea habari na chanzo cha mimi kulazwa hosipitali. Daktari akajibu, " Ikiugu, husitie ukunguru wala kubabaika na haya mambo. Unagua malaria ambayo karibu yaharibu bongo lako ijapo sasa kila kitu iko barabara". Haya matamshi yalionekana kuwafurahisha wageni wangu, haswa mpenzi wangu aliyekuwa na shaka chungu nzima kuhusu maisha yetu ya usoni.
Wageni wote, ikiwemo dada yangu na mpenzi wangu waliangaliana kwa namna ya kuashiria ya kwamba walikuwa wanashuku ya kwamba nilikuwa na ugua malaria. Hii ni sababu nilikuwa mkonde kama sindano, mifupa ilikuwa nje, macho ndani kama mbegu za maembe na uzito wangu ulikuwa mdogo sana kuliko dama aliyezaliwa jana. Niliunyoosha mkono wangu wa kulia na kumshika dada yangu huku nikumueleza na kumudhibitishia ya kuwa, sina ukimwi kama walivyodhani. Thibitisho ya kuwa ni malaria wala sio ukimwi ilifanya nyuso zao kutoa miale ya tabasamu na nderemo.
Muda wa kuwaona wagonjwa ulikuwa unayoyoma na kila mmoja wao alikuwa katika hali ya kuniaga kwaheri. Shangazi yangu aliinua mkono wake wa kushoto juu bali akiuwekelea mkono wake wa kulia kifuani mwangu. Maombi yakaanza kabla ya wao kuchapa kaguu hadi nje ya chumba cha wagonjwa. Wakati huu wote, nilikuwa nahisi mchanganyiko wa uchungu na baridi mwili mzima hadi sehemu nyeti. Hali niliyokuwa uume wanguhaungeweza kuinuka hata kama yule daktari mrembo angenipakata na kunishikashika. Hali haingeruhusu.
Usiku huo, nililala kichalichali huku mafikira chungu nzima ya kijaa akilini mwangu. Moja yapo ya mafikira ni mbona ugonjwa ulinipata punde tu nilifanikiwa kupata tunzo la kwenda kusoma shahanda ya utafiti kwa miezi sita huko ng'ambo? Nilishuku nimerogwa na jirani moja ambaye roho yake ilikuwa chafu zaidi ya nguruwe. Shetani ni mmbaya lakini Mwenyezi Mungu hali sima.
Saa moja ya jioni usiku huo, bado kama nimejilaza pale kwa kitanda kichalichali, niliwaona wanawake wanne, wamejivaa nguo refu refu za rangi nyeupe. Walikuwa wakicheka huku wamebeba sitrecha; kile chombo cha kuwabebea wagonjwa. Macho zao zilikuwa zang'aa kama dhahabu.Walikuwa na nywele mrefu, umbo la kutamani na tabasamu isiyo kifani. Sitrecha ilikuwa imetengenezwa kwa mbao. Nilikuwa nadhani niko ndotoni lakini la. Hawa walikuwa Malaika wa Mungu. Niliwatasama tu sababu singeweza kutoa sauti. Niliwasikia tu wakineneshana kwa lugha ambayo sikuelewa.
Walinibeba kwa hiyo sitrecha na kunipeleka mahali mbali ambapo sikujua. Waliponiweka kulikuwa na mwangaza mingi na nyota za kumetameta. Kulikuwa na watu wengi pia wenye nguo nyeupe na mabawa. Niliona nyufa za dhahabu, maua ya kupendeza na picha za Yesu za dhahabu. Pale chini waliponiweka, mmoja wa hao malaika akaunyoosha mkono wake na kutoa kitu ambacho sikujua ni nini hapo karibu na roho yangu. Hiyo sehemu alitoa kitu ndipo uchungu ilikuwa imezidi sana. Katika ile pilka pilka ya kutoa kitu hapo kifuani mwangu, ghafla nilijihisi mwenye nguvu, furaha na uchungu yote kuisha. Baadaye, wale wanawake wanne wakanibeba tena kwa sitrecha na kunirudisha hospitalini.
Maajabu, kesho yake punde daktari alipowasili kunitazama na kuchukua vipimo, alipigwa na bumbuazi kuona hali yangu ilivyo endelea tu baada ya siku moja baadaye. Kwa mshangao wake, nilijitoa kitandani bila usaindizi wake, nikasimama kando ya kitanda kama mlingoti na kudai kwenda nyumbani. "Sina uchungu daktari", nilimueleza. Daktari, akaniruhusu kwenda nyumbani. Akawapigia dada yangu na wazazi wangu waje kunichukua.
Familia mzima ilikuja wakiandamana na padre wawili mmoja akiwa ameshika bibilia na mwenzake msalaba. Pindi walipofika, mwangaza mweupe ukawaka katika chumba cha wagonjwa. Halafu nikasikia sauti kama ya Mungu ikisema.........TO BE CONTINUED
Comments
Post a Comment